Home » » Kampuni ya Uber kutengeneza magari yanayopaa

Kampuni ya Uber kutengeneza magari yanayopaa

Written By Bizzi on Monday, April 17, 2017 | April 17, 2017


Muhandisi wa zamani wa shirika la maswala ya angani Nasa ameajiriwa na kampuni ya teksi Uber kusaidia katika utafiti wake wa kutengeza magari yanayoruka.

Mark Moore anajiunga na Uber kama mkurugenzi wa uhandisi wa angani.

Lengo la Uber katika kutengeza magari yanayoruka lilianza mwezi Oktoba ambapo maswala ya kupaa na kutua yalijadiliwa.

Uber tayari inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na Daimler.

Katika mipango yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapunguzia wateja wake muda wanaopoteza kila siku wanaposafiri.

Mpango huo utashirikisha mtandao wa ndege za kielektroniki ambazo zitapaa na kushuka wima.

Moore alisema mpango kama huo katika jarida lililochapishwa wakati alipokuwa Nasa.

Alisema kuwa mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango huo ni betri zitakazotumika.

Kampuni ya kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruka ambayo inatarajiwa kuingia katika soko mwaka huu.
Share this article :

No comments:

Post a Comment