Recent

FAQ's

Powered by Blogger.

Facebook

Technology

Business

Gadgets

Search This Blog

Blog Archive

Videos

Technology

Sports

Fashion

Business

Header Ads

Social

Contact Form

Name

Email *

Message *

Categories

Advertise Here

Tags

Nature

Comments

Popular

Popular Posts

Jose Chameleone anunua pair ya kiatu yenye thamani ya Milioni 25 za kitanzania

Written By Bizzi on Monday, April 17, 2017 | April 17, 2017

Ile tabia ya watu maarufu kununua vitu vyenye thamani imeendelea kuongezeka kwa kasi hivi sasa, ambapo Jose chameleone mwanamziki anayetokea UGANDA ametrend kwa kuonyesha viatu vyake viwili vyenye thamani ya dola za kimarekani 12,500.

Jose chameleone amesema kununua viatu hivyo hamaanishi kwamba anajionyesha ila ni moja ya njia anayotumia kumshukuru Mungu.

Jose Chameleone akiwa amevishika viatu hivyo
Jose ni mmoja kati ya wanamuziki wenye mafanikio zaidi kwa wakati huu, ambapo utajiri wake amekuwa akiuweka wazi mara kwa mara kwa kuonyesha magari na nyumba anzozimiliki.

Wavuta bangi wapata kanisa lao,litafunguliwa siku ya bangi duniani April 20


Wapenzi wa bangi na kuabudu wamepata kanisa lao, kanisa hili lipo mjini Denver Marekani na litafunguliwa April 20 ikiwa ni siku ya wavutaji duniani.
Taasisi ya dini Elevation Ministries imetangaza uzinduzi wa kanisa hili la kimataifa International Church of Cannabis, ikiwa ni sehemu ya wavutaji kujiskia huru kuabudu.

Waumini wa kanisa hili wanajiita Elevationists, na Jengo la kanisa hili linamiaka 113 na limerekibishwa hivi karibui…

2 Chainz amesha kubali kufanya show kwenye uzinduzi wa kanisa hili.

Forbes yatoa orodha ya wasanii wapya wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi 2017


Forbes imeachia orodha mpya ya wasanii wapaya wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi “Forbes Hip-Hop Cash Princes”
Kwenye Oorodha hiyo wapo Bryson Tiller ambaye alikuwa akiingiza $100,000 kwa usiku mmoja kwenye tour yake ya muziki huku akiingiza nyimbo mbeli zilioongoza kwenye chart ya Top 40 na album yake ya TrapSoul ikiwa imeenda Platnum,Desiigner mbali ya nomination ya Tuzo za Grammy, Ngoma yake ya Pandaimeongoza chart nyingi ikiwemo Billboard Hot 100 na pia emepata dili nono la kusainiwa kwenye lebel ya Kanye West G.O.OD Music.

Hii ndio orodha kamili,
Desiigner
D.R.A.M.
Tory Lanez
Lil Uzi Vert
Lil Yachty
Noname
Isaiah Rashad
Stormzy
Bryson Tiller
Young M.A.

Mwaka jana Boi-1da, DeJ Loaf, Fetty Wap, G-Eazy, Joey Bada$$, Lil Dicky, Logic, na Metro Boomin walitajwa kwenye orodha hiyo.

Hawa ndio Waigizaji 20 wa filamu wanaolipwa zaidi duniani

Forbes wametoa orodha mpya ya waigizaji wa filamu wa kiume wanaolipwa fedha zaidi duniani.

Dwayne ‘The Rock’ Johnson ndiye ameongoza orodha hiyo Lakini pia kwenye orodha hiyo kuna waigizaji wa kiwanda cha filamu cha Bollywood,

20. Harrison Ford – $15m
19. Matthew McConaughey – $18m
18. Amitabh Bachchan – $20m
17. Will Smith $20.5m
16. Chris Pratt $26m
15. Leonardo Dicaprio $27m
14. Salman Khan – $28.5
13. Mark Wahlberg $30m
12. Adam Sandler $30m
11. Brad Pitt – $31.5m
10. Akshay Khumar $31.5m
9. Robert Downey Jr – $33m
8. Shah Rukh Khan – $33m
7. Vin Diesel – $35m
6. Ben Affleck – $43m
5. Johnny Deep – $48m
4. Tom Cruise – $53m
3. Matt Damon – $55m
2. Jackie Chan – $61m
1. Dwayne ‘The Rock’ Johnson $64m

Hii ndio listi mpya ya matajiri 10 duniani iliyotolewa na Forbes


Jarida linalofatilia maisha ya watu maarufu na mali zao “Forbes” limetoa list ya watu matajiri zaidi duniani, na wakati huu kuna mabadiliko makubwa ya watu waliofanikiwa kuingia kwenye Top 10. Bilionea Bill Gates ameendelea kushika nafasi ya kwanza ikiwa ni mara ya 18 kati ya 23 zilizowahi kutajwa.

Kijana mfanyabiashara wa mitandao Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa mitandao maarufu ya kijamii kama Facebook, Whatsapp na Instagram amepanda mpaka nafasi ya 5 mwaka huu.

Hii ndio listi nzima ya matajiri wa dunia.

Aliyekuwa kiongozi wa Freemason Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia


Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande amefariki Dunia.

Sir Andy Chande alikuwa mwanachama wa Freemason kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora,Tanzania.

Jeshi la Polisi limewaua majambazi waliowaua askari 8 Kibiti


Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwani jana usiku.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

Polisi anayedaiwa kumuua mwenzake asakwa kwa dau

“Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Kampuni ya Uber kutengeneza magari yanayopaa


Muhandisi wa zamani wa shirika la maswala ya angani Nasa ameajiriwa na kampuni ya teksi Uber kusaidia katika utafiti wake wa kutengeza magari yanayoruka.

Mark Moore anajiunga na Uber kama mkurugenzi wa uhandisi wa angani.

Lengo la Uber katika kutengeza magari yanayoruka lilianza mwezi Oktoba ambapo maswala ya kupaa na kutua yalijadiliwa.

Uber tayari inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na Daimler.

Katika mipango yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapunguzia wateja wake muda wanaopoteza kila siku wanaposafiri.

Mpango huo utashirikisha mtandao wa ndege za kielektroniki ambazo zitapaa na kushuka wima.

Moore alisema mpango kama huo katika jarida lililochapishwa wakati alipokuwa Nasa.

Alisema kuwa mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango huo ni betri zitakazotumika.

Kampuni ya kutengeza magari ya ya Aeromobil kutoka nchini Slovakia ni miongoni mwa kampuni ambazo zina mpango wa kutengeza gari la kuruka ambayo inatarajiwa kuingia katika soko mwaka huu.

YAJUE MAMBO 11 KUHUSU IKULU YA MAREKANI(WHITE HOUSE)

Kuna mambo mengi usiyoyajua kuhusu ikulu ya marekani ambayo pengine kwa msomaji anaweza kushangazwa akiyajua.Hivyo katika kusherehekea Sikukuu ya Rais baadhi ya watu waliweza kutoa mambo 11 kuhusu ikulu ya Marekani ambayo ina jumla ya vyumba 132 na imejengwa katika eneo la ukubwa wa mita za mraba 17,000. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

Awali ilijulikana tu kama jengo la West Wing ni ofisi za watendaji. West Wing ilijengwa na Rais Teddy Roosevelt akiwa na lengo la kutenganisha makazi na sehemu za ofisi. Hata hivyo alipoingia madarakani Rais Taft akaamua kuunganisha jengo la ofisi la West Wing na majengo ya makazi akisema anataka kuhusika zaidi na shughuli zzote za White House.

Ndani ya ikulu ya Marekani kuna nyumba pacha ambapo inaelezwa kuwa James Hoban ni mbunifu na raia wa Ireland alichora kwa mfano wa jengo la Leinster la jijini Dublin huko Ireland. Awali jengo la Leinster lilikuwa makazi ya kiongozi wa Leinster na kwa sasa ni jengo la bunge la Ireland. Kwa maneno mengine White House ya Marekani inashabihiana na jengo la bunge la Ireland.

Katika ikulu ya marekani hakuna kitu kama chakula cha bure, hata kwa Familia ya rais wa nchi hiyo.Mwishoni mwa kila mwezi, Rais anapata bili yake binafsi ya kulipia chakula chake na familia yake ikiwa ni pamoja na huduma zote zinazotolewa ndani kama kufanya usafi, dawa ya meno, na vifaa vya vyoo, ambayo hukatwa kutoka katika mshahara wake dola 400,000 kila mwaka.

Watu wengi wanajua kuhusu eneo la Bowling lakini kuna mambo mengine kadhaa ya kuvutia katika eneo la chini ya White House. Ukiachilia chumba cha ‘situation’ ambacho hutumiwa na rais wa Marekani pindi kunapotokea dharura ya kitaifa au kimataifa kuna vitu kama duka la maua, karakana ya mafundi seremala, na ofisi ya daktari wa meno kiasi kwamba rais hana sababu ya kutoka nje ya White House kwa shida yoyote ile. Kila kitu kimo ndani ya ikulu ya Marekani.

Ikulu ya marekani imekuwa ya kushangaza kwa kuwa moja ya taasisi maarufu duniani. White House kila wiki inapata hadi wageni 30,000 na barua 65,000. Aidha karibu simu 3,500 hupigwa, barua pepe 100,000, na faksi 1000 hupokelewa katika ikulu hiyo ya Marekani kwa wiki.

Pamoja na ukweli kuwa Ikulu ya marekani hairuhusu kuingilia faragha za Raisi pamoja na familia yake ambao hutumia simu maalumu bado huwezi kuweka hakikisho la mia kwa mia kuwa baadhi ya mazungumzo ndani ya ikulu ya Marekani huvuja.

Ikulu ya marekani ilijengwa kwa msaada wa watu wengi. wasanii wengi wa Ulaya na wafanyakazi wahamiaji ikiwa ni pamoja na waashi kutoka Scotland. Matofali na plasta ilifanywa na wafanyakazi kutoka Ireland na Italia. Katika hali ya kusikitisha historia za kumbukumbu za mishahara zinaonyesha wajenzi wengine walikuwa watumwa wamerekani wenye asili ya Afrika.

Jina la White House halikuwa likitumiwa hapo kabla hadi alipoingia madarakani rais Theodore Roosevelt ndipo ikulu hiyo ikapewa jina hilo. Awali ikulu hiyo ilijulikana kama kasri la watendaji.


Kama ilivyo kwa majengo yoyote makubwa duniani, mauzauza hayakosekani na miongoni mwa mauzauza hayo kubwa ni lile la rais Winston Churchill kukataa kulala tena katika master bedroom ya Lincoln baada ya mzimu wa Lincoln kumtokea rais Churchill ambapo alimwona ameketi kando ya tanuru chumbani alipotokeza kutoka kuoga.

White House daima imekuwa katika mabadiliko ambapo awali haikutarajiwa kuchaguliwa kwa rais mlemavu na ilipotokea ilibidi kurekebisha milango na kujengwa kwa lifti ili kumwezesha rais mlemavu kutembelea maeneo yote ya ikulu ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa bwawa maalumu la matibabu kwa rais huyo mlemavu.

Katika ajabu la kumi na moja rais Clinton alifanya marekebisho ya ikulu ya aina yake. Yeye alijenga baseni la kuogea lenye maji moto lenye ukubwa wa kutosha watu saba. Pia kulikuwa na uwezekano wa watu wawili tu kutumia beseni hilo.

Mke wa Roma Mkatoliki Afunguka Tena


Mke wa msanii Roma Mkatoliki Nancy Mshana (kushoto) akiwa na mume wake.

Mke wa msanii Roma Mkatoliki Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.

Nancy ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana .Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki

Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.

“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy

Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

KASHFA ZAZIDI KUMWANDAMA ZUMA PRETORIA, AFRIKA KUSINI

CHAMA cha upinzani cha Congress of the People (Cope) kinapanga kumshitaki Rais Jacob Zuma kwa kumpatia ulinzi maalumu kwa viongozi wa ngazi za juu (VIP) aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma.

Dk. Dlamini-Zuma alipewa ulinzi wa VIP kufuatia madai ya kutishiwa maisha, ambayo polisi walikuwa wakiyachunguza.

Mwingine atakayehusishwa katika kesi hiyo ni Waziri mpya wa Polisi, Fikile Mbalula.

Cope ilieleza hatua hiyo ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi na ni haramu na kinyume cha Katiba.

“Dk. Dlamini-Zuma si mgombea urais wala mbunge anayestahili kupewa ulinzi wa VIP ambao ni maalumu kwa maofisa waandamizi wa serikali na wakuu wa mataifa wa kigeni na wake zao,” kiongozi wa Cope Mosiuoa Lekota, alisema katika taarifa.

Alisema analaani vikali vitendo vya ukiukaji sheria na Katiba vinavyofanywa na Rais Zuma na Mbalula.

“Zuma na Mbalula wanapaswa kufikishwa mahakamani kueleza sababu ya matumizi haya mabaya ya fedha za walipa kodi ‚” alisema Lekota.

Kauli ya Lekota imekuja baada ya Jeshi la Polisi kufichua Zuma aliyetangaza nia ya kuwania urais wa Chama tawala cha Africa National Congress (ANC) na ambaye ni mke wa zamani wa Rais Zuma aliendelea kupokea ulinzi wa VIP kutokana na uchunguzi unaoendelea kuhusu vitisho vilivyoelekezwa kwake.

Msemaji wa Jeshi la Taifa la Polisi Sally de Beer alikiri kuwapo kwa ulinzi wa ziada.

Lakini Meja Jenerali De Beer alikataa kueleza kiundani kuhusu aina ya ulinzi aliopewa Dk. Dlamini-Zuma na aina ya vitisho alivyopokea.

Dk. Dlamini-Zuma anaonekana kuwa na nia ya kumrithi mumewe huyo wa zamani na ameshaanza kampeni.

Aidha amekuwa mstali wa mbele kumtetea Rais Zuma dhidi ya wakosoaji wanaomtaka ajiuzulu kutokana na mlolongo wa kashfa za ufisadi, upendeleo na ubadhilifu.

WAMAREKANI WAMTAKA TRUMP ATANGAZE KODI ALIYOLIPA SERIKALINI


MAKUMI kwa maelfu ya watu katika miji mbalimbali nchini hapa wameendesha wakitaka Rais Donald Trump atangaze kodi aliyolipa kwa Serikali, jambo ambalo yeye binafsi amekataa kulifanya.

Waandamanaji wengine walibeba sanamu kubwa za kuku, wakimaanisha Rais ni mwoga na amekataa kutoa takwimu za kodi yake.

Karibu watu 14 wametiwa mbaroni huko Berkeley katika jimbo la California ambako wafuasi wa Rais Trump na wapinzani wake walikabiliana.

Ingawa hakuna sheria inayomlazimisha Trump kutangaza kodi yake, marais wote wa Marekani wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda wa miongo minne iliyopita.

Maandamano hayo yalipangwa kwenda sambamba na siku ya mwisho ya raia kuwasilisha takwimu zao za kodi.

VIJANA WATAKIWA KUJITAFUTIA FURSA


Na HARRIETH MANDARI,

VIJANA nchini wametakiwa kubadili mtazamo wa kuwa ajira ndiyo njia pekee ya kuwainua kiuchumi na badala yake wajikite kwenye sekta isiyo rasmi kwa kuanzisha biashara mbalimbali.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Athony Mavunde, ameyasema hayo hivi karibuni, wakati akifungua mafunzo ya uhamasishaji wa ujasiriamali kwa vijana wa jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri huyo alisema, bado vijana wengi wana mtazamo kuwa ajira ndiyo njia pekee ya kuwa na maisha bora na ya uhakika.

Alisema takwimu za vijana walio kwenye sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi nchini ya mwaka 2014, zinaonyesha vijana walio kwenye sekta rasmi ni kati ya 850,000 -1,000,000,000 na walio bado kwenye soko la ajira ni 150,000-200,000 na hivyo kuweka pengo la vijana zaidi ya 600,000 ambao hawana cha kufanya.

“Kama Serikali, tumekuwa tunachukua hatua kuondokana na changamoto hiyo ambapo imeanza kuwawezesha vijana mmoja mmoja na vikundi,” alisema Mavunde.

Alisema kuwa, tatizo linalokwamisha kundi hilo ni kukosa vigezo vya kukopesheka kwenye mabenki, hivyo kuwalazimu kukaa vijiweni bila kazi, japokuwa wengine tayari wana mawazo na mipango mizuri ya biashara.

“Lipo kundi la vijana ambao pamoja na kuwa hawakufanikiwa kusoma hadi ngazi za elimu ya juu, lakini wana vipaji vya ufundi, kilimo na vingine vingi, ambao pia serikali imeandaa mkakati wa kuwakwamua kiuchumi kupitia vipaji vyao,” aliongeza.